Robert A. Macdonald, C.Ss. R.
Imeandikwa na
SKAPULARY YA KIJANA


Fatima Network Online

Hebu niwaeleze hadithi ya jinsi nilivyoigundua Scapulari ya kijani, Hii ni njia pekee ya kujaribu kusambaza ukweli na mapendo ya dhati; ya moyo wa huruma wa Mama yetu na pia njia ya kufanya malipizi kwake. Mnamo miaka michache iliyopita kabla ya matumizi ya penisilini nililazwa hospitalini kwa kuumwa sana na ugonjwa wa kichomi.

Nilianza kutokwa damu na madaktari wakaamua kunifanyia operesheni kama ndiyo njia ya mwisho. Baada ya uamuzi huo akaingia mtawa mdogo wa kike chumbani mwangu na kuniuliza.

“Padre. Unayo imani kubwa kwa Mama wa Mungu na hasa katika moyo wake safi kabisa? Kama ndio unaweza ukapona.

“Kwa namna gani”

“kwa njia ya Scapulari ya kijani”

“Scapulari ya kijani ni nini?

“Padre miaka minne iliyopita nilipata operesheni ya kutokana na ugonjwa wa kansa. Ikagunduliwa kuwa ugonjwa huo ulishaenea mwilini mwangu kiasi kwamba waliamua tu kunishona na kunitoa nikafe. Hatimaye nikasali kwa Mama yetu wa scapulari ya kijani nikachoka kusubiri kifo na nikarudi kazini, nimepona, padre. Ungependa nikupe scapulari?

“Tafadhali nipatie Sista”

Mara moja akaiweka moja juu ya kichwa changu. Nikajawa na imani kubwa sana na damu ikakoma kunitoka. Siku mbili baadaye katika chumba cha X-ray wakaniuliza lini damu iliacha kutoka. Nilipowajibu kuwa imeacha siku chache zilizopita walishangaa sana.

“Unakidonda ambacho kimepona miezi sita iliyopita na hakuna hata alama. Leo hata makovu yamepotea. Ndio maana ninasema ninalo deni lisilolipika kwa moyo safi wa Mama yetu. Kuanzia hapo nimekuwa nafanya kila liwezekanalo ili kutekeleza mapenzi hayo.

Kwa furaha kubwa na mshangao nimeona kuwa wale wote niliowaeleza suala la skapulari ya kijani wamekuwa waadilifu zaidi kuliko mimi. Sijawahi kuwaona watu wenye imani kuzidi hawa wafuasi wapya wa Mama maria.

Mnamo mwezi wa May nilimuomba Gombelo wa Mtakatifu Patrick Toronto anipe ruhusa niweze kuongea wakati wa ibada ya Jumatano. Nilikuwa na Skapulari za kijani elfu moja na hakuna hata mmoja aliyedhani kwamba zaidi ya thelathini zinahitajika. Lakini zote elfu zimalizika siku ya kwanza. Chumba tulichokuwa tunagawia Skapulari hizo kilijaa pomoni kiasi kwamba niliogopa uwezekano wakupatikana majeruhi. Kwa siku nzima nilisingirwa na wateja wakihitaji Skapulari zaidi. Kwa upumbavu wangu nikawaonyesha ya kwangu na mara moja ikanyanganywa kutoka mikononi mwangu.

Wanaweza wakaeleza vizuri zaidi kuliko mimi hadithi ya Sista ambaye alihamasisha mapendo na kuigwa na yeyote aliyekutana naye. Mtu aliyekuwa anaaminika sana na Papa Pius wa tisa (9) katika siku zile za giza kabla hajafungwa kule Vatikan aliyekuwa anahusudiwa na Waislamu wa Afrika Kaskazini na aliyekuwa anapewa kilemba cha ukoka akilinganishwa kama Mama maarufu Florence Nightingale kwenye viwanja vya vita vya Crimea. Wanaweza wakakueleza jitihada alizozifanya kwanza yeye mwenyewe asijulikane na jinsi hatimaye siri yake ilivyojulikana.

Watarudia maelezo ya Mama wa Mungu akisimama katika uzuri wake wote mbele ya kijana “Novice” mara kwa mara hadi Skapulari ikatengenezwa na kusambazwa.Alimwachia ujumbe yule Sista kijana kuwa Skapulari inaweza kubarikiwa na Padre yeyote na mtu anaweza kutembea nayo au kuivaa na hata akaiweka tu chambani kwake.

Nguvu maalum ya Skapulari ni uwezo wake wa kubadili mioyo ya binadamu na hatimaye kumweka mwanae katika mioyo hiyo.

Sala muhimu ambayo inaweza kusemwa na pia kumwombea mwingine inasema “Moyo safi wa Maria utuombee sasa na saa ya kufa kwetu” Miaka kumi baada ya maono ya medali ya kimujiza kwa Sista Catherine Laboure mnamo mwaka 1830, Mama mbarikiwa alikabidhi Skapulari ya kijani ya moyo mtakatifu kwa Sista Justine Bisqueyburu ambaye ni binti wa ukarimu wa Mtakatifu Vincentde Paul.

Jinsi ya kutumia Skapulari ilionyeshwa na Bikira mbarikiwa.Kwa vile Skapulari siyo beji ya uanachama wa imani moja bali ni taswila mbili katika kipande cha nguo kinachoingizwa kwenye kamba basi kutabaruku hakutakiwi. Inatosha tu ikibarikiwa na padri na kuvaliwa na yeyote anayehusika. Skapulari inaweza kuwekwa kwenye nguo, kitandani au ndani ya chumba.

Sala muhimu ni maandishi ya upande wa pili wa Skapulari yaliyozunguka moyo ambayo yanasema “moyo safi sana wa Maria Utuombe sasa na saa yakufa kwetu”

Ingawa rehema za ajabu hupatikana kutokana na Skapulari lakini ni wazi kuwa rehema hizo hupatikana kwa uwiano wa imani yako juu ya Skapulari.

Skapulari ya kijani iliidhinishwa mara mbili na Papa Pius wa tisa mwaka 1863 na 1870 wakati aliposema kuwa waandikieni hawa masista kuwa nimetoa kibali kwao watengeneze na kusambaza Skapulari.

September, 18, 1962
Archibishop of Baltimore
Nihil obstat: E.A. Cerry, s.s. S.T.D.
Taarifa za mabadiliko na kupona kutokana na Skapulari ya kijani zikieleza muda, mahala na mtu anayehusika zipelekwe kupitia anwani zifuatazo

Kwa taarifa zaidi na Catalog ya vitabu vya dini pamoja na kanda za dini piga simu Toll-Free l-800-263-8160 au andika kwa anwani zilizoonyeshwa hapa juu.

!E-mail kwetuZaidi maswali kuhusu Fatima?


Nyuma ya Kwanza kuu
Copyright 1996 - 2013 The Fatima Network